AFRIKA kuna historia kubwa lakini ujinga ulisamaa juu ya urithi huu. Mwanahistoria mmoja wa Kiingereza aliwahi kusema kuwa, Afrika kuna historia ya Ulaya tu. Zeinab Badawi amekuwa akijiuliza nini kipo nyuma ya huku kutokujua na anaitazama mfululizo wa historia hii ya Mwafrika kati BBC World News.
Piramidi kubwa la Giza mjini Cairo limechukuliwa kama moja ya maajabu saba ya dunia kwa ulimwengu wa kale. Lakini ukisafiri zaidi kusini mwa Mto Nile utakuta maelfu ya mapiramidi yanayosadikiwa kuwa ni ya Ufalme wa Kush, ambayo sasa inajulikana kama Sudan.
Kush ulikuwa utawala wenye nguvu wa Kiafrika na msukumo wake umeendelea mpaka sasa huko kunakojuikana kama Mashariki ya Kati.
Ufalme huu umedumu kwa mamia ya miaka katika karne ya nane kabla ya Kristu (BC), uliushinda ule wa Misri na kutawala kwa kipindi kirefu cha karne.
Nini kimebaki katika utawala huo ni cha kushangaza. Zaidi ya mapiramidi 300 bado hayabomoka, hayajaguswa tangu yamejengwa karibu miaka 3000 iliyopita.
Zeinab Badawi

"Kuna njia ya kuitazama Afrika katika nyanja ya umasikini na migogoro ambayo imekuwa ni kielelezo kwa bara hilo ambacho kinabaki mpaka sasa."
Baadhi ya mifano bora kabisa inaweza kupatkana kule Jebel Barkal, Kaskazini mwa Sudan , imetangazwa kama na Unesco kuwa ni urithi wa dunia.
Hapa utakuta mapiramidi, makaburi, mahekalu na vyumba vya kuzikia vyenye michoro na maandishi ambayo Unesco imeyaelezea kama kazibora ambazo hazitokuja kutokea (masterpieces) "za ubunifu wa akili nyingi zinazoionesha sanaa, jamii, siasa na dini za makundi ya watu kwa zaidi ya miaka 2000".
AFP
Miaka kadhaa iliyopita nilitembelea haya mapiramidi. Na nilipokuwa narudi Uingereza niliuliza wazazi wangu kitu gani wanajua kuhusu maeneo ya kihistoria ya nchi yao.
Hii haikuwa ajabu tangu kwani wote wawili wangeweza kukueleza mengi kuhusu Henry VIII na mambo muhimu ya historia ya Waingereza.
Nimeshangaa kuwa wazazi wangu walikuwa hawajui mengi kuhusu historia ya nchi yao na hii naweza kusema ndivyo ilivyo kwa Waafrika wengi.
Na nilipoongea na watu wengine nikagundua kuwa tatizo ni lilelile.
Miaka michache baadae, katika makao makuu ya Unesco, jijini Paris, katika kabati la vitabu la Makamu Mkurugenzi Mkuu, Getachew Engida, mzaliwa wa Ethiopia, mkusanyo wa vitabu vya General History of Africa.
Hii, ilikuwa ni moja ya siri ambazo Unesco imejiwekea na maalumu kwa bara la Afrika: Historia ya Afrika iliyoandikwa na msomi Mwafrika.

Mradi huu ulianzishwa mapema miaka ya 1960 wakati wa kujitawala kwa Afrika. Baadhi ya viongozi huru wa Kiafrika waliamua kuwa baada ya kujitawala katika nchi zao pia wajitawale katika historia zao.
Wanahistoria wa Maghalibi wamelalamikia ukosefu wa kumbukumbu za kutosha za baadhi ya historia zilizoandikwa za nchi za Kiafrika na wakatumia hii kama sababu ya kukataa hilo.
Unesco imewasaidia wasomi wa Afrika kuweka pamoja miradi yao, kuajiri wataalamu 350, wengi wao kutoka Afrika na wenye nidhamu, kutengeneza matoleo nane, kuanzia historia ya kimaandishi mpaka ya kisasa.
Toleo la nane lilikamilika mwa 1990 na la tisa bado linafanyiwa kazi.
Unesco ilichukua hatua ya utata ya kuanza kuandika toleo kwa kuanzia na historia ya mwanadamu, kwa kuweka nadharia ya mageuzi ya binadamu (evolution). Kwa kufanya hivyo, wamengesababisha hasira kwa Wakristo na Waislamu katika nchi za Afrika ambako wapo, na wanaendelea kuwepo huku wakiendeleza imani ya uumbaji.

Mwanapalaeontolojia wa Kenya, Richard Leakey, ambaye amechangia kwenye toleo la kwanza, amesema, yeye anaamini kuwa ukweli kuwa mwanadamu asili yake ni Afrika anapingana na Wamaghalibi, ambao wanaukana uasili wao wa Kiafrika.
Historia ya Utawala wa Kush, wenye nguvu katika Asia ya Maghalibi sawasawa na Afrika, ambako Malkia ametawala kwa haki yao wenyewe, pia mara nyingi umepuuzwa.
Hii pia ni kweli kuwa Utawala wa Aksum, umejieleza kuwa ni mmoja kati ya jamii kubwa za ulimwengu wa kale.
Wafalme wa Aksum walikuwa wakiongoza biashara katika Bahari Nyekundu kuanzia katika ardhi yao ambayo kwa sasa ni Eritrea na Ethiopia. Pia walikuwa watawala wa kwanza katika Afrika kuukumbatia Ukristo na kufanya kuwa dini rasmi katika falme zao.
Hii ni historia ijulikanayo wa uchache, kote Afrika na kwingineko, kwa sababu wanataaluma wengi na waalimu katika nchi za Kiafrika ni zao la elimu za kikoloni, na hivyo hawawezi kupokea na kutetea historia yao.

Wazazi wangu Wasudani wanaongea Kiingereza, na wameelimika sana, lakini kwa upana sana wamefundishwa kwa mitaala ya Kimaghalibi.
Hata walipokuwa wakitazama hiastoria yao, bado waliitazama kwa mtazamo wa usomi wa Kimaghaibi.
Moja ya mtazamo huo ilirejelea misemo ya Hugh Trevor-Roper, anajulikana kama mmoja wa wanahistoria wa Kiingereza.
Alisema mwaka 1965: "Labda katika nyakati zijazo, kutakua na historia ya Waafrika ya kufundisha. Lakini kwa sasa hakuna, au ipo kidogo: Kuna historia ya Wazungu waliowahi kuwepo Afrika tu."
"Kilichobaki ni giza, kama historia ya Wazungu wa awali, Waamerika Wakolumbia wa awali. Na giza si jambo la kihistoria."
Ukweli ni kwamba ni watu wachache wanaojua juu ya matoleo haya yaliyotengenezwa chini ya Unesco kuwa yanakwambia kitu fulani. Ushangae kwa nini viongozi hawataki kung'aa kwa jambo hili.
Hili lingekuwa jambo jema kwa Afrika, kwa sababu lingetukuza kufikia hatua ambayo haijawahi onekana mahali popote duniani.
Imetafsiriwa kutoka BBC

Comments
Post a Comment