Mwanvlogu wa Senegal anayeishi nchini Marekani amefurushwa nchini humo.
Assane Diouf anayejulikana kwa machapisho yake ya mara kwa mara katika mtandao wa YouTube pamoja na ukosoaji wa rais Macky Sall na viongozi wa dini wa Senegal mbali na viongozi wa kisiasa.
Bwana Diouf anayesema kuwa anamuunga mkono mtangulizi wa Macky Sall Abdoulaye Wade ni miongoni mwa raia wa Senegal waliofurushwa nchini Marekani kwa kuwa nchini humo kinyume na sheria.
Maafisa wa polisi wa Senegal wamethibitisha kwamba bwana Diouf anazuiliwa na maafisa wa jinai katika mji mkuu wa Dakar.

Comments
Post a Comment